Wananchi wa Kata ya Mnolela inayojumuisha vijiji 6 pamojana vitongoji vyake, wanatarajia kunufaika na huduma za afya zinatolewa katika zahanati ya Mnolela ifikapo mwezi June 2017. Hali hiyo imetokana na usaidizi wa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alitoa mchango wake binafsi kwa zahanati hiyo pamoja michango mingine iliyotolewa na Mh. Mbunge wa Jimbo la Mtama Mh. Nape M. Nnauye pamoja na wadau wengine ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Lindi.
Zahanati ya Mnolela ilipata bahati ya kutembelewa na msafara wa Mh. Rais akiwa katika ziara za kikazi kutembelea mikoa ya Lindi na Mtwara na kuweza kusimamishwa na wananchi wa eneo hilo na kusikiliza kero zao hasa huduma za afya zinazotokana na kukosekana kwa huduma bora za uzazi ikiwemo kukwama kwa ujenzi wa jengo la kujifungulia akina mama wajawazito. Pia ujenzi huo unahusisha jengo la upasuaji mdogo, jengo la uzazi, choo pamoja na korido.
Ujenzi na upanuzi wa zahanati hiyo unatekelezwa na kusimamiwa na Wakala wa Ujenzi wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kushirikiana na Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi pamoja na Kamati ya Afya ya zahanati hiyo. Ujenzi unaendelea vizuri na inategemewa kufunguliwa na kuanza kufanya kutoa huduma mwishoni mwa mwezi Juni 2017.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.