Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi:Zuwena Omari ametoa pongezi za dhati kwa Menejimenti nzima ya Halmashauri ya Wilaya ya Mtama kwa kupata hati safi kwa miaka mitano mfululizo, Ameyasema hayo leo juni 18 ,2025 katika kikao maalumu cha Baraza kwa lengo la kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali(CAG), Kikso hiko kimefanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo Halmashauri ya Mtama.
Akiongea na wajumbe wa kikao Bi:Zuwena Omari alisema kuwa kupata hati safi siyo jambo dogo bali ni jambo kubwa ambalo limehusisha umakini wa watu, utekelezaji wa majukumu, uwajibikaji pamoja na ushirikiano mkubwa, lakini pia ameitaka Menejimenti ya Halmashauri ya Mtama kuhakikisha inalinda hati safi zilizopatikana kwa miaka mitano mfululizo.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe: Victoria Mwanziva amewapongeza waheshimiwa madiwani na timu nzima ya CMT Halmashauri ya Mtama kwa kufanya kazi kwa bidii ya kuhakikisha kero za wananchi zinatatuliwa kwa wakati lakini pia kwa kuhakikisha miradi yote ya maendeleo inaenda vizuri na viwango vinavyostahili ili kuleta maendeleo.
Hata hivyo Mwenyekiti wa kikao hiko Mhe: Yusufu Tippu amewapongeza Waheshimiwa madiwani, Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Mkurugenzi Mtendaji na wataalamu wa Halmashauri kwa kushiriki ipasavyo kikao hiko maalumu lakini pia amesisitiza kila kiongozi kutimiza wajibu wake ili kujenga na kuboresha Halmashauri ya Mtama.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.