Mafunzo hayo yamefanyika Leo tarehe 26 Machi 2025 katika ukumbi wa Heinberk uliopo Nyangao, Lengo la mafunzo hayo ikiwa ni kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa mazingira ili kuhakikisha wanatumia nishati safi ya kupikia ili kuokoa muda pamoja na kupunguza gharama za matumizi.
Akitoa neon la ufunguzi wa mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndugu Mwinjuma Muumini alisema kuwa washirii wa mafunzo hayo wanatakiwa kuhakikisha wanapeleka elimu waliyoipata katika jamii zinazo wazunguka.
Aidha Bwana Emmanuel Msuya mwezeshaji wa mafunzo hayoamewataka wadau hao kuhakikisha wanapata uelewa sahihi kuhusu umuhimu wa Nishati safi na mbadala kwa matumizi mbalimbali kama vile kupikia.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.