Rai hilo limetolewa 24 Februari, 2022 na Mratibu wa Maafa Halmashauri ya Mtama Ndg. Ismail Mbani akiambatana na Afisa Utumishi Mohamed Kalunga walipotembelea na kuwafariji waathirika wa mvua na kuwaomba baadhi ya wananchi ambao nyumba zao zimeharibiwa kwa kiasi kikubwa kuhama kwani nyumba hizo sio salama kwa makazi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mtendaji wa Kata ya Nyengedi Ndg. Thomas Ngomo inaeleza kuwa mvua hiyo iliyoambatana na upepo mkali ilitokea usiku wa tarehe 23 Februari, 2022 kuanzia saa 6:22 usiku hadi saa 9:25 alfajiri na kusababisha kutokea kwa maafa ya uharibifu wa nyumba 113 kwa kukatika kuta na nyingine kubomoa viwambaza vya nyumba.
Aidha kufuatia mvua hiyo baadhi ya wananchi wamekosa makazi na kulazimika kuhifadhiwa kwa ndugu zao na kwamba hakuna mtu yeyote aliyeumia ama kufariki.
Baadhi ya nyumba zilizoathiriawa na mvua
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.