Katika ufunguzi huo, mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mtama Ndg. George Mbilinyi aliwapongeza vijana hao kwa kuchaguliwa kuwa miongoni mwa wakusanyaji wa taarifa za Anwani za makazi huku akiwasisitiza kuwa mabalozi wa kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa zoezi hilo, kufanya kazi kwa umakini na weredi, pamoja na kuwa na uzalendo katika utekelezaji wa shughuli hiyo kwani kwa kufanya hivyo itakuwa ni chachu ya kushirikiana kwenye shughuli nyingine za kiutendaji.
Mafunzo hayo ya siku mbili yanayotolewa kwa makundi tofauti yanafanyika kwenye ukumbi wa shule ya sekondari Nyangao na yanatarajiwa kufungwa tarehe 16, Machi 2022.
Box 328 Lindi
Postal Address: 328 Lindi Dc
Telephone: 0222061
Mobile:
Email: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.