Leo Machi 08, 2022 ikiwa ni siku ya wanawake duniani, walimu wanawake kupitia Idara ya Elimu Msingi na Sekondari wameadhimisha siku hiyo kwa kuwatembelea wanafunzi wenye mahitaji maalumu shule ya msingi Nyangao na kuwakabidhi zawadi ikiwa ni pamoja na sabuni za kufulia, kuogea, sabuni za chooni, mafuta ya kupaka, biskuti, pipi na pedi kwa wanafunzi wa kike kwa lengo la kuwafariji na kuwatia moyo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mtama, Ndg Hassan Nungu ametoa shukurani kwa walimu hao kutokana na moyo wao wa kuwakumbuka watoto hao huku akiongeza kuwa wanafunzi hao wana haki ya kupata elimu katika mazingira mazuri hivyo wasichoke kuwasaidia ili watimize ndoto zao.
Kufuatia tukio hilo, mwanafunzi Azimina Rashidi alipata nafasi ya kutoa shukurani kwa walimu hao na kuwakaribisha tena katika viwanja vya shule hiyo.
Maadhimiyo hayo yanakwenda sambamba na kauli mbiu " KIZAZI CHA HAKI NA USAWA KWA MAENDELEO, TUJITOKEZE KUHESABIWA"
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.