Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Zainab Telack amewataka Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama kuendelea kusimamia miradi inayotekelezwa kwa ukaribu na kuhakikisha wanaweka nguvu ya kutosha kwenye usimamizi wa miradi hiyo.
Ameyasema hayo jana tarehe 3 Machi 2025 katika ziara yake ya kutembelea na kukagua Miradi ya ujenzi wa miundombinu ya Elimu katika Halmashauri ya Mtama.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya kata Hingawali unaogharimu TZS 560,552,827 ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya kanda Kiwalala unaogharimu TZS 4,100,000,000 ujenzi wa shule ya Sekondari ya kata Mtakuja unaogharimu TZS 560,552,827 na ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Mtakuja.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.