Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 22 Aprili 2024 katika shule ya msingi Mihogoni kwa lengo la kutoa chanjo kwa watoto wa kike kuanzia umri wa miaka 9 hadi 14 ili kuwakinga na ugonjwa hatari wa saratani ya mlango wa kizazi lakini pia zoezi hilo litakuwa endelevu kuanzia leo tarehe 22 Aprili hadi tarehe 28 Aprili 2024, Chanjo hiyo itaenda kuwafikia watoto wa kike 11812 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama ikiwa ni zaidi ya asilimia 80.
Akiongea na wanafunzi wa kike katika shule hiyo Bi Juliana Kikoti ambaye ni mlezi wa Halmashauri alisema kuwa kinga ni salama kuliko tiba kwani chanjo hiyo itaenda kuwakinga watoto dhidi ya ugonjwa huo ambao unasababishwa na kirusi cha HPV lakini pia aliwataka wanafunzi hao kuwa mabalozi kwa wasichana wengine waliopo majumbani kwani chanjo ni salama.
Aidha Diwani wa kata ya Mtama Mheshimiwa Maria Nyale aliwapongeza waalimu kwa malezi bora ya watoto lakini pia idara ya Afya chini ya Mganga mkuu wa Halmashauri na kuwaomba idara hiyo chanjo zijazo kuwashirikisha wazazi ambao wapo jirani ili kuondoa dhana potofu kwa jamii kuhusu chanjo hizo na kuwataka wanafunzi wachanje bila wasiwasi kwani chanjo ni bora na salama
Mgeni Rasmi wa zoezi hilo Mheshimiwa Athumani Sefu Hongonyoko Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Lindi aliwataka viongozi pamoja na wananchi kumuunga mkono Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa nguvu kubwa katika sekta ya Afya kwani ana maono ya mbali kwani bila Afya hamna Taifa imara na aliongeza kuwa saratani itapungua kwa asilimia kubwa kupitia chanjo hizi zinazotolewa leo, Mwisho mgeni Rasmi alizindua chanjo hizo ili kutolewa kwa wanafunzi hao na jamii kwa ujumla.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.