Wadau na viongozi mbalimbali katika Mkoa wa Lindi wamefanya kikao kazi Cha sekta ya Elimu katika mji mkongwe wa Kilwa Masoko kuanzia tarehe 28-30 disemba 2020. Wadau hao walifanya tathimini kwa kupitia changamoto na namna ya kujipanga kwa kuweka mikakati ya mwaka 2021. Aidha katika kikao hicho Cha maabara ya Elimu, Afisa Elimu mkoa Mwl Vicent Kayombo alitoa taarifa ya maendeleo ya Elimu mkoa wa Lindi na mkoa umeshika nafasi ya kwanza kitaifa kwa miaka 2 mfululizo kidato Cha 6 na darasa la Saba kushika nafasi ya 14 kitaifa na darasa la 4 nafasi ya 10. Kikao hicho kilikabidhi vikombe vya ushindi kwa Komredi Christopher Ngubiagai -Mkuu wa Wilaya Kilwa ambaye alimwakilisha RC - LINDI. Kila Halmashauri imejiandaa vema kupitia mipango mkakati yao chini ya Kauli mbiu " Uwajibikaji wangu katika kuinua Elimu bora na ufaulu mkoa wa Lindi". Kikao hicho kimesimamiwa na Bi Rehema S. Madenge Katibu Tawala Mkoa wa Lindi.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.