Kikao Cha viongozi wa Elimu katika ngazi ya Halmashauri sita za Mkoa wa Lindi pamoja na wadau wengine wa Elimu wamefanya tathimini ya Elimu ya Msingi na Sekondari kwa kupitia mipango mkakati ya Mwaka 2019 kwa kuangalia mafanikio na changamoto zilizopo na hatimaye kutengeneza mpango mkakati wa utekelezaji kwa Mwaka 2020.
Wajumbe kwa pamoja walipata nafasi kubwa ya kuchangia mada zote zilizotolewa katika kikao hicho kilichofanyika Tarehe 17-18/12/2019 katika ukumbi wa mikutano katika shule ya Sekondari ya WAMA SHARIF iliopo Manispaa ya Lindi. Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi Dr. Bora Haule katika ufunguzi aliwaomba wajumbe wawe na ushirikiano,umoja na ushirikiano katika ufuatiliaji wa tendo la ufundishaji na ujifunzaji kwa ngazi zote . Kama kila mmoja akitimiza wajibu wake basi tuna imani kubwa kwa Mwaka 2020 Mkoa utafanya vizuri zaidi kuliko Mwaka huu 2019.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.