Mdau wa michezo Ndg Selemani Methew Luwongo amekabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 4 na laki 6 kwa timu zilizoshiriki na baadhi ya timu za mpira wa miguu za Mtama . Vifaa hivyo ni pamoja na jezi za netball na mpira wa miguu, mipira na nyavu za magoli amevigawa leo tarehe 15 Agosti 2021 katika Bonanza la 'NANI KAMA MAMA TOURNAMENT' katika viwanja vya Bomeni Mtama.
Bonanza hilo liliandaliwa na kuratibiwa na mdau wa michezo kwa kushirikiana na viongozi wa michezo wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama na Kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo afisa michezo Wilaya ya Mtama Masoud Mohamed Elewa pamoja na Walimu wa michezo shule za msingi na sekondari. Washiriki wakuu wa bonanza hilo walikua timu ya netball ya Veterani ya kata ya Majengo na Mtama, Timu ya netball Ya Dada's kata ya Mtama, timu ya netball ya Mtama sekondari, timu ya netball Mahiwa sekondari, timu ya netball ya shule ya msingi Mihogoni na timu ya netball shule ya msingi Mtama na michezo mbalimbali ilichezwa, huku lengo kuu likiwa ni kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji na michezo ya wanawake pamoja na kuleta hamasa na kujenga afya bora miongoni mwao.
Washiriki wa bonanza wakiburudika
Kabla ya kukabidhi vifaa hivyo, mdau huyo wa michezo alipata nafasi ya kuzungumza na washiriki ambapo amesema kuwa lengo la kutoa vifaa hivyo ni kuhakikisha halmashauri ya wilaya ya Mtama inakua zaidi kimichezo pamoja na kuibua vipaji mbalimbali katika jamii. Aidha Ameahidi kufufua na kurekebisha viwanja vya michezo ili viwe katika hadhi ya viwanja vya kiwiilaya hivyo basi amesistiza zaidi kwa washiriki wa bonanza hilo kuithamini na kuipenda michezo kwani michezo ni ajira lakini pia ni njia bora ya kuimarisha afya zao. Sambamba na hayo Ndg Luwongo ametoa wito kwa wenyeji na wadau wengine Wa michezo wajitokeze kwa wingi ili kuwezesha kusonga mbele katika sekta ya michezo.
Nae Afisa michezo Wilaya ya Mtama Masoud Mohamed Elewa ameahidi kufufua na kuendeleza michezo kupitia uwanja huo wa Bomeni lakini pia ametoa wito kwa washiriki wote waliopatiwa vifaa vya michezo kuvitunza vifaa hivyo ili vitumike katika siku zijazo.
Zoezi la ugawaji huo wa vifaa vya michezo litaendelea katika tarafa mbalimbali ndani ya Halmashauri ikiwemo tarafa ya Sudi, Rondo, pamoja na tarafa ya Nyangamara.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.