Kiongozi wa mbio za Mwenge maalumu wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi , tarehe 27 Agosti 2021 ametembelea miradi 7 ya maendeleo Wilaya ya Lindi ambapo miradi 2 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama na miradi 5 Halmashauri ya Manispaa ya Lindi kwa lengo la kukagua na kuweka mawe ya msingi pamoja na kufanya uzinduzi katika miradi wa utoaji wa huduma za afya kwa mfumo wa Got-homis kwenye kituo cha afya cha Mnazi Mmoja.
Aidha miradi iliyotembelewa na mwenge huo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama ni pamoja na ujenzi wa barabara ya Mtama hadi mahakama ya mwanzo mita 800 kwa kiwango cha lami pamoja na mradi wa ujenzi wa maabara na matundu ya vyoo 6 katika shule ya sekondari Mtua.
Akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Mtama hadi mahakama ya mwanzo Mtama mkurugenzi wa TARURA Wilaya ya Lindi Eng. Dawson Paschal, amesema mradi huo ni miongoni mwa miradi mitano ya barabara inayotekelezwa na wakala wa barabara vijijini na mijini (TARURA) katika Halmashsuri ya Wilaya ya Lindi kwa mwaka wa fedha 2020/2021 ambao umegharimu kiasi cha Tsh. 296,690,000/= kwa awamu ya kwanza na tayari mkandarasi amelipwa kiasi cha Tsh. 271,550,000/= na kubaki kiasi cha Tsh. 25,140,000/= . Ameongeza kuwa kwa mwaka wa fedha 2021/2022, mradi huo umetengewa kiasi cha Tsh. 80,150,000.00/=ambazo zitatumika katika utekelezaji kwa awamu ya pili. Aidha Eng. Dauson ameeleza kuwa, mradi huo ulianza tarehe 20 Januari 2021 na kukamilika tarehe 30 Agosti 2021 ambao umetekelezwa kwa awamu ya kwanza chini ya utekelezaji wa mkandarasi wa M/S SERC Constructin Ltd na kwamba mradi huu utapangiwa fedha kila mwaka ili kuweza kukamilika kwa usanifu wake.
Kukamilika kwa mradi huu kutasaidia watumiaji wa zahanati ya Mtama, Mahakama ya mwanzo lakini pia ni mpango na jitihada za kuboresha miji inayokua katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama.
Mradi mwingine ni ujenzi wa maabara ya sayansi na matundu sita ya vyoo katika shule ya sekondari Mtua ambao umetolewa taarifa za utekelezaji wake na mkuu wa shule hiyo Mwl.William Kanyondo na kusema mradi huo ulianza mwaka 2014 kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri pia ni miongoni mwa miradi 23 kupitia mpango wa Lipa kwa Matokeo ambao utagharimu kiasi cha Tsh 62,000,000/=hadi kukamilika kwake. Aidha ameeleza kuwa mradi huo umepokea Tsh 40,000,000/=za EP4R kutoka serikali kuu na Tsh 22,000,000.00/= kutoka Halmshauri ambapo kiasi cha Tsh. 15,000,000/= Za Halmashauri zimetumika katika ujenziwa vyumba viwili vya maabara na kiasi cha Tsh. 7,000.000/= zinatumika kwenye ujenzi wa matundu 6 ya vyoo vya wanafunzi na kwamba jumla ya Tsh. 56,075,639/= zimetumika na Tsh. 5,924,361/= zinzendelea kutumika katika shughuli za umaliziaji.
Sambamba na hilo kiongozi wa mbio maalumu za Mwenge wa Uhuru 2021 Luteni Josephine Mwambashi ametembelea miradi mitano katika Halmasahuri ya Manispaa ya Lindi ikiwemo mradi wa mfumo wa Got-homis katika kituo cha afya cha Mnazi Mmoja wenye gharama ya shilingi 34,524,500/=, mradi wa vyumba sita vya madarasa na matundu ya vyoo nane katika shule ya msingi Mnazi Mmoja uliogharimu shilingi 116,920,000/=, ametembelea mradi wa maji wa Tandangongoro wenye gharama za Tsh. 2,726,843,628.61/=, ametembelea mradi wa vikundi vya wajasiriamali vya wanawake, vijana na walemavu wenye jumla ya gharama ya Tsh 2,726,843,682.61/= lakini pia ametembelea mradi wa kituo cha mfumo wa taarifa za Kijiografia wenye thamani ya shilingi s123,529344/=
Aidha, wakati akitoa salamu na ujumbe wa Mwenge wa Uhuru 2021 kwa wananchi wa Wilaya ya Lindi, kiongozi wa mbio maalumu za Mwenge alieleza mambo muhimu ikiwemo matumizi ya malipo ya kielektroniki wakati wa ukusanyaji wa mapato kwa ngazi ya Halmashauri na kusisitiza zaidi kuhusu umuhimu wa risiti ya EFD. Lakini pia amewahasa wananchi juu ya matumizi sahihi ya TEHAMA huku akisisitiza zaidi kuwa na ushirikiano katika mapambano dhidi ya rushwa, malaria, UKIMWI, matumizi ya dawa za kulevya pamoja na ugonjwa wa COVID19 kwa la kuwa na taifa endelevu.
Katika Wilaya ya Lindi, jumla ya miradi 7 imetembelewa ambapo miradi 3 imezinduliwa, miradi 3 imewekwa mawe ya msingi na mradi mmoja umetembelewa. Mbio maalumu za Mwenge wa Uhuru 2021 zimehitimishwa tarehe 28 Agoti 2021 ukiambatana na kauli mbiu “TEHAMA NI MSINGI WA TAIFA ENDELEVU ITUMIE KWA USAHIHI NA UWAJIBIKAJI”.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.