Katibu tawala wa mkoa wa Lindi, Mhe. Zuwena Omari, leo tarehe 08, Januari 2025 ametembelea na kukagua hali ya miradi mbalimbali ya kimaendeleo inayosimamiwa na serikali na kutekelezwa na Halmashauri ya wilaya ya Mtama.
Miongoni mwa miradi iyo ni ujenzi wa shule ya msingi mtakuja, ujenzi wa shule ya sekondari mpenda na ujenzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya kanda inayojengwa Kiwalala, Halmashauri ya wilaya ya Mtama huku hali ya miradi iyo ikiwa katika hatua za awali.
Aidha, mbali na kutembelea na kukagua miradi ya kimaendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Mtama vile vile kuangalia maandalizi ya mapokezi ya wanafunzi wanaotarajiwa kuanza masomo yao mwaka 2025.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.