Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndugu Yusufu Tipu leo tarehe 13 machi 2024 ameambatana na kamati ya maafa ya Halmashauri Kwa lengo la kutoa msaada wa chakula ikiwa ni unga kilo 475 na maharage kilo 50 Kwa waathirika wa mafuriko katika kata ya Nyangao.
Aidha Afisa Mazingira wa Halmashauri Ndugu Ismaili Mbani Kwa niaba ya Mkurugenzi alisema Kuwa Serikali inaendelea kuwapa moyo na kuwafariji wahanga hao Kwa kidogo ambacho wamekitoa na kuahidi kushirikiana Kwa pamoja katika kipindi hiki kigumu wanachopitia.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Kijiji hiko Ndugu Erick Muhaji Kwa niaba ya wananchi ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mheshimiwa Rais Daktari Samia Suluhu Hassan na Halmashauri Kwa ujumla kwa kuendelea kuwajali Wananchi wa Nyangao kwa maafa waliyoyapata na kuona umuhimu wa kuwaletea msaada wa vyakula hivyo.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.