Halmashauri ya Wilaya ya LINDI inaendelea na ratiba yake ya kutoa huduma za matibabu ya kibingwa katika vituo vyake.
Huduma hiyo imepangwa kufanyika katika Kambi nne ndani ya Halmashauri ya Lindi/Mtama. Kambi hizo ni Hospitali ya Misheni Nyangao, Kituo cha Afya Nyangamara, Kituo cha Afya Kitomanga na Kitui cha Afya Rondo Chiponda.
Huduma hiyo inatolewa na Madaktari Bingwa wa ndani ya Halmashauri ya LINDI wanaopatikana katika Hospitali na vituo vyake, wataalamu hao ni pamoja na Bingwa wa Magonjwa ya Moyo, Bingwa wa magonjwa ya Masikio, pua na koo, Bingwa wa magonjwa yanayohitaji upasuaji na Bingwa wa magonjwa ya uzazi na akina mama.
Mganga Mkuu Wilaya ya LINDI Dr. Dismas Masuluhu alisema huduma hiyo inatolewa kwa lengo la kuwasogezea huduma wananchi ambao wapo mbali na hospitali kubwa na wana matatizo ambayo wengi wanashindwa kujihudumia kutokana na gharama kubwa za matibabu. Huduma hiyo inatolewa kwa gharama ndogo ya shilingi 5,000 ambayo ni kwa ajili ya kumuona Daktari, ushauri na matibabu.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya LINDI Bw. Samweli Warioba Gunzar amewataka wananchi wa LINDI na maeneo ya jirani kutumia fursa hiyo adhimu ili kupata huduma kwa tarehe zilizopangwa.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.