Mhe: Victoria Mwanziva Mkuu wa Wilaya ya Lindi amewasisitiza Wananchi wa kata ya Majengo Halmashauri ya Mtama kuhakikisha wanatenga kipato Chao maalumu Kwa ajili ya kurekebisha mazingira ya vyoo na makazi Kwa ujumla kwani choo bora hulinda faragha pamoja na afya lakini pia huzuia magonjwa ya milipuko kama kuhara na homa za matumbo.
Ameyasema hayo Jana tarehe 19 Disemba 2024 katika Maadhimisho ya Siku ya choo duniani yaliyofanyika katika viwanja vya sokoni-Majengo ndani ya Halmashauri ya Mtama, Aidha Maadhimisho hayo yamefanyika Kwa lengo la kutoa elimu Kwa Wananchi kuhusu umuhimu wa kuwa na choo bora nyumbani na hata katika taasisi za Umma.
Lakini pia wadau kutoka Heart to Heart foundation pamoja na wadau kutoka Angalikana Jimbo la Masasi waliungana pamoja katika Maadhimisho hayo ili kuhakikisha elimu ya utumiaji wa choo bora inawafikia Wananchi wote wa kata ya Majengo na Halmashauri ya Mtama Kwa ujumla.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.