Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe: Victoria Mwanziva ameyasema hayo Leo tarehe 26 Aprili 2025 alipowasilisha ujumbe maalumu wa Muungano Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe: Zainab Telack, Maadhimisho hayo yamefanyika kimkoa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama ndani ya viwanja vya Shule ya Sekondari Nyengedi.
DC Mwanziva aliongeza kuwa Muungano huu umetoa fursa Kwa Wana Lindi kuishi Kwa Amani na kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo pamoja na kushirikiana na Wananchi wa Zanzibari katika nyanja zote za kisiasa, kiuchumi na kijamii, lakini pia Muungano huu unaendelea kuwa nyenzo na utambulisho muhimu wa umoja na mshikamano ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha Maadhimisho hayo yaliambatana na zoezi la upandaji wa miti ya matunda na kivuli katika eneo maalumu ndani ya Shule ya Sekondari Nyengedi Kwa Lengo la kuweka kumbukumbu ya kudumu ya Maadhimisho hayo ya 61 katika Shule hiyo.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.