Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe: Victoria Mwanziva Leo tarehe 04 Novemba 2024 ameongoza kikao maalumu Cha tathmini ya lishe Kwa lengo la kujadili, kupokea na kutathmini hali ya lishe katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama, kikao hiko kimefanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo Halmashauri ya Mtama.
Aidha Mwenyekiti wa kikao hiko ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi amewataka watendaji wa kata kuhakikisha kuwa shule angalau mbili katika Kila kata zinakuwa na bustani za uhakika Kwa ajili ya mbogamboga pamoja na matunda.
Akitoa Tathmini ya Lishe Kwa wajumbe wa kikao hiko Ndugu Gozbert Henerico Mratibu wa Iishe Wilaya alisema kuwa Kila shule hasa Kwa shule zilizipo maeneo ya karibu na huduma ya mashine zinatakiwa kutumia mashine maalumu za kuchanganya vyakula na lishe ili kuhakikisha Wanafunzi wanakula vyakula bora na vyenye lishe kamili.
Lakini pia Ndugu Hudhwaifa Rashidi Katibu Tawala Wilaya ya Lindi amesisitiza uwepo wa hamasa na vikao vya mara Kwa mara Kwa wazazi ambao bado hawaoni umuhimu wa kuchangia chakula mashuleni kwani mzazi anajukumu la kuhakikisha mtoto wake anapata chakula shuleni na nyumbani.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.