Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe:Victoria Mwanziva ameongoza na kuzindua Rasmi hafla ya utoaji wa mikopo ya 10% katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama inayotolewa katika ngazi za Halmashauri kupitia mapato ya ndani, Hafla hiyo imefanyika leo tarehe 10 Februari 2025 katika ukumbi wa mikutano uliopo Halmashauri ya Mtama.
Akitoa taarifa ya utoaji wa mikopo hiyo Ndugu Wenceslaus Mbilango Afisa Maendeleo ya Jamii alisema kuwa vikundi 52 vya wanawawake, vijana na watu wenye ulemavu wanatarajia kupatiwa fedha Shilingi Milioni miatatu sitini laki tano thelethini na tisa elfu (360,539,000) ikiwa ni vikundi vya wanawake 32, vijana 16 na watu wenye mahitaji maalumu 14.
Akiongea na wawakilishi wa vikundi vilivyonufaika na mikopo hiyo DC Mwanziva amewataka kuwa na nidhamu ya fedha ikiwa ni pamoja na kutochanganya fedha za mikopo na matumizi binafsi badala yake fedha hizo ziende kuimarisha uchumi wa wajasiriamali hao na kuleta chachu ya maendeleo.
Kwa upande wa wanufaika wa mikopo hiyo wameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais DKT: Samia Suluhu Hassan na uongozi wa Halmashauri kwa ujumla kwa kuona umuhimu wa kuwapatia mikopo hiyo ambayo haina riba kwani itaenda kuinua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.