Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe: Victoria Mwanziva kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi amewapongeza wataalamu wa afya Mkoa wa Lindi kwa jitihada za kuhakikisha vifo vya mama na watoto wachanga vinapungua, ambapo katika Mkoa wa Lindi vifo vya mama vitokanavyo na uzazi vimepungua kutoka vifo 38 mwaka 2023 hadi kufikia vifo 27 mwaka 2024 lakini pia vifo vya watoto wachanga chini ya siku 28 vimepungua kutoka 272 mwaka 2023 hadi kufikia vifo 242 mwaka 2024.
Ameyasema hayo jana tarehe 12 Machi 2025 katika ufunguzi wa kikao kazi cha kujadili vifo vya mama vitokanavyo na uzazi pamoja na watoto wachanga kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo Shule ya Sekondari Nyangao huku lengo la kikao hiko ikiwa ni kujadili mikakati ya kupunguza vifo hivyo.
Aidha DC Mwanziva amempongeza kwa dhati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake na uwekezaji mkubwa uliofanyika katika sekta ya afya uliosaidia mafanikio hayo ya kupunguza idadi ya vifo ndani ya mwaka mmoja, jitihada hizo ni pamoja na ujenzi wa hospitali ya Mkoa, ujenzi wa hospitali mpya za Halmashauri ikiwemo hospitali ya Wilaya ya Mtama iliyopo Kiwalala pamoja na marekebisho mbalimbali katika vituo vya afya na zahanati.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.