Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Mtama labariki na kupitisha bajeti ya shilingi bilioni 34 kwa mwaka wa fedha 2025/2026 ambapo bilioni 5 kutoka kwenye mapato ya ndani na bilioni 29 kutoka Serikali kuu, Bajeti hiyo imepitishwa jana tarehe 11 februari 2025 katika mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano uliopo Halmashauri ya Mtama.
Akihutubia Baraza hilo Mkuu wa Wilaya ya Lindi MHE: Victoria Mwanziva alipongeza uongozi wa Halmashauri ya Mtama ukiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe: Yusufu Tippu kwa kuandaa bajeti nzuri ambayo imegusa sekta zote, Aidha DC Mwanziva amewataka wataalamu wa Halmashauri kusimamia utendaji wa maendeleo kwa fedha ambazo zimetengwa.
Hata hivyo, Ndugu Anderson D Msumba Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mtama alisema kuwa 40% ya bajeti hiyo itaelekezwa kwenye sekta ya kilimo aidha katika kuongeza mapato ya Halmashauri pia bajeti imelenga kuendeleza ujenzi wa stendi ya kituo cha mabasi Mtama lakini pia bajeti itaelekezwa katika sekta ya elimu kwa wanafunzi ambao wanakosa fursa ya kuendelea na masomo kwa kukosa vifaa kama sare na madaftari.
Kwa upande wa Waheshimiwa Madiwani wameipokea vizuri bajeti hiyo na kusisitiza vipaumbele hasa kwa TARURA kuhakikisha wanaimarisha miundombinu ya barabara lakini pia pembejeo za kilimo zifike kwa wakati kila kata.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.