Baada ya kupokea kesi ya ugonjwa wa mahindi ambao hapo awali haukujulikana jina lake, Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Bi. Vaileth Richard Byanjweli amefanya jitihada za kufuatilia na kubaini kuwa ugonjwa huo kitaalamu unaitwa Corn Smut Disease unaoathiri zao la mahindi na kuwa katika hali ya fangasi.
Amesema kuwa ugonjwa huo unaweza kusambaa kutoka hindi moja kwenda lingine na kusababisha athari kubwa kwenye zao hilo na kwamba tatizo hilo halijawahi kutokea katika Halmashauri ya Mtama.
Bi vaileth ameongeza kuwa tatizo Hilo hutokea Kwa kutokutumia mbegu bora zilizothibitishwa na Wataalamu pamoja na kutokufata Kanuni bora za kilimo.
Aidha amewataka wakulima kuzingatia Kanuni bora za kilimo kwa kuwa karibu na Wataalamu wa kilimo ili kupata elimu kuhusu zao husika huku akiwasisitiza kutoa taarifa pindi tatizo lolote linapotokea kwa lengo la kulipatia ufumbuzi.
Katika hatua za awali za kukabiliana na tatizo hilo, wakulima wanashauriwa kuondoa mahindi yaliyoathirika ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.
Ugonjwa huo uligundulika tarehe 4 Novemba 2021 kwenye shamba la mahindi la Bi. Maua Mohamedil ililopo katika Kijiji cha Mvuleni Kata ya Mtama na kuathiri baadhi ya mazao hayo.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.