Watu wengi wamekuwa na mazoea ya kutumia mifuko ya plastic maarufu kama rambo kwa ajiri ya kubebea vyakula vya moto kama vile ugali,supu,chips mayai bila ya kujua athari ambazo wanaweza kupata walaji wanaofunga vyakula vyao kwa vifungashio hivi, na pia kuna athari za Mazingira zinazotokana na matumizi ya Mifuko hii ya plastic yalibainishwa na ndugu Lewis Nzali. Mratibu wa Mazingira wa kanda ya Kusini
Mifuko hii ya plastic haifai kuwa vifungashio vya chakula kwani ikipata joto kwa muda mrefu hutoa kemikali ambazo hujulikana kwa jina la Polyvinly chloride na stylene ambazo huingia kwenye chakula na hivyo huingia mwilini kwa njia ya mtu unapokula na kama mtu huyu atakuwa na mazoea ya kula kwa vyakula hivi kwa kutumia vifungashio hivi vya plastic basi kemikali hizi huendelea kujrundikana mwilini na hivyo humpelekea mtu kupata saratani..
Mbali na uwezekano wa kuugua ugonjwa huo wa saratani pia kuna madhara mengine ambayo mtu utaweza kuyapata ni kubadili mfumo wa jeni za mwili ambayo hupelekea matatizo ya uzazi Moya na matatizo ya kushindwa kuweka katika msawazo,vichochea vya mwili kutokuwa sawa,kizunguzungu nk
madhara haya hayatokei haraka haraka bali hutokea baada ya muda fulani ndipo huanza kujionesha kidogo kidogo kwa hivyo ni heri kupunguza matumizi haya ya mifuko ya plastic ili tuweze kujiokoa sisi wenyewe na vizazi vyetu kama unataka chakula cha moto ni heri kwenda na Hot pot ndogo ya kuhifadhia chakula hicho, Mazingira ni wajibu katika kila mmoja wetu kama kila mtu atatekeleza wajibu wake ipasavyo tuyalinde
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.