Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Mh. Yusuph Abdallah Tipu ambaye pia ni Diwani Kata ya Nyengedi Machi 3, 2022 amefanya ziara ya kikazi kutembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa shule ya sekondari Chiponda pamoja na ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mtegu.
Katika ziara yake amewataka wajumbe wa kamati za ujenzi pamoja na mafundi kuhakikisha wanafanya kazi kwa uaminifu, weredi kasi zaidi kwa kuzingatia viwango vinavyoendana na thamani ya fedha iliyotolewa.
Ujenzi huo unaendelea ukiwa katika hatua ya msingi kwa baadhi ya majengo ikiwa ni pamoja na jengo la maktaba na kazi zinaendelea.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.