Kupanga, kusanii mradi, kujenga na kusimamia uendeshaji na matengenezo ya miradi ambayo imeshajengwa.
Kufanya ukaguzi wa miradi ya maji ambayo imejengwa
Kutoa Elimu ya uvunaji wa maji ya mvua
Kusimamia mapato na matumizi ya mfuko wa maji
Kutoa mafunzo ya mafundi wa vijijini ili wawe na uwezo wa kufanya matengnezo madogo pindi inapobidi.
Kutoa elimu pamoja na kusimamia upandaji wa miti rafiki ya maji katika vyanzo vya maji
Kuandika mapendekezo (Project proposal) ya miradi ya maji kama uvunaji wa maji ya mvua, ujenzi wa visima virefu, maji ya kutega (gravity scheme) na kukinga maji ya chemichemi (spring protection).
Kusimamia uanzishwajni wa jumuiya za watumiaji maji na kufanya maandalizi na maadhimisho ya wiki ya maji
Kufanya ukaguzi wa visima virefu na vifupi vijijini kila baada ya miezi mitatu (Quarterly Inspection).
Kufanya mikutano ya Hadhara, ili kutoa maelekezo ya sera ya maji juu ya uanzishwaji wa jumuiya za watumiaji maji na michango ya maji yenye tija kwa ajili ya matengenezo ya miraid ya maji.
Kusimamia mafunzo ya mafundi wa vijijini (Pump Attendants) ili wawe na uwezo wa kufanya matengenezo madogo pindi yanapotokea.
Kusimamia mapato na matumizi ya mfuko wa maji.
Kusimamia uendeshaji na matengenezo ya miradi ya maji iliyokwisha jengwa.
Kusimamia uendeshaji na matengenezo ya miradi ya maji iliyokwisha jengwa.
Kusimamia ufunguaji wa Akaunti za maji Benki
Kusimamia miundombinu mipya ya maji-: Matanki ya maji (Water storage tank) Intakes, Vituo vya kuchotea maji (Water points), Matanki ya chini ya kupunguza msukumo wa maji (Break pressure tank) na Utandikaji wa mabomba kutoka kitega maji.