Kupitia/kuendeleza na kutafsiri malengo ya kilimo ya wilaya, sera na mikakati sambamba na sera na miongozo ya kitaifa.
Kuwa na utaratibu wa kuendeleza na kutoa miongozo kwa wadau wa kilimo ( mashirika yasiyo ya kiresikali, mashirika ya kijamii) na kuyahusisha kwa kuyajengea uwezo katika utoaji huduma wilayani.
Kuhakikisha kuwa maandalizi ya miradi ya maendeleo ya kilimo wilayani yanalenga kutatua changamoto za walengwa kwa kuwa inaandaliwa kwa mbinu shirikishi.
Kuwa katika mstari wa mbele katika uwajibikaji utoaji wa huduma kwa mteja kwa kuhakikisha taratibu zinafutwa na maamuzi yanafanyika kwa wakati, na kujihusisha na utoaji wa zabuni kwa mikataba.
Kuwezesha mawasiliano mazuri kati ya vituo vya utafiti, ugani na wakulima/vikundi vya wakulima na kuwa kiungo na watumishi wa kilimo wilayani, kata na vijijini na watumishi wa idara nyingine.
Kuhakiki, kutoa maelekezo, na kusambaza taarifa za utafiti kwa walengwa wote (wakulima) wilayani.
Kusukuma na kuimarisha uhusiano na taasisi na mashirika yanayojihusisha na maswala mtambuka katika wilaya mfano; mazingira, ukimwi, jinsia na utunzaji wa maliasili na kuhakikisha kuwa maswala hayo yanahusishwa katika mipango endelevu wa kilimo.
Kuratibu na kushauri juu ya shughuli zote za kilimo kufanyika kwa ushiriano wa sekta rasmi na isiyo rasmi (mashirika binafsi). Kusimamia na kuunganisha taarifa matukio ya majanga na wadudu/visumbufu vya mazao vinavyo/yanayotukia katika kanda, mkoa, na taifa kwa ujumla.
Kushirikiana na idara za serikali na maafisa wa serikali za mitaa katika kushauri, kuendeleza na kuhamasisha utekelezaji wa sheria ndogo za kilimo.