Halmashauri ya Wilaya ya Mtama imepokea na kukimbiza Mwenge wa Uhuru Jana tarehe 26 Mei 2025 katika miradi 7 ya maendeleo yenye thamani ya Shillingi Bilioni 2.7 inayotekelezwa katika Halmashauri ya Mtama, Mwenge wa Uhuru umekimbizwa Kwa umbali wa KM 153.
Miradi iliyopitiwa ni pamoja na Mradi wa kituo cha Afya Pangaboi kilichopo kata ya Nachunyu wenye thamani ya Shillingi milioni 500, Mradi wa Shule ya Sekondari pangatena wenye thamani ya Shillingi milioni 560, 552, 827, Mradi wa kikundi Cha vijana wa bodaboda kilichopo Nampunga kilichonufaika na mkopo wa asilimia 10 kutoka Halmashauri, Mradi binafsi wa shule ya Awali ya ST.Leonard Kiwalala wenye thamani ya Shillingi milioni 200, Mradi wa kituo cha stendi ya mabasi Mvuleni- Mtama wenye thamani ya Shillingi milioni 900 lakini pia Mradi wa barabara ya Lihimba- Mtama wenye thamani ya Shillingi milioni 522, 263,750 wenye umbali wa M 600 Kwa kiwango Cha lami.
Aidha kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Comrade Ismail Ali Ussi amesema kuwa Miradi yote iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru Halmashauri ya Mtama imeridhiwa Kwa asilimia 100, hii inaonyesha kuwa Mhe: Mbunge wa Jimbo la Mtama, Waheshimiwa Madiwani pamoja na Viongozi wa Halmashauri ya Mtama wanafanya kazi kubwa ya kuwatumikia Wananchi lakini pia kumpa heshima Rais DKT: Samia Suluhu Hassan.
Hata hivyo, Halmashauri ya Wilaya ya Mtama imemaliza kikamilifu tukio hilo la Kitaifa( kukimbiza Mwenge wa Uhuru) na kwenda kuukabidhi Mwenge huo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi katika viwanja vya Shule ya Msingi Mnazi Mmoja.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.