Kukagua na kutoa ushauri sahihi ili kuboresha utawala bora
Kufanya ufuatiliaji na ukaguzi na usimamizi wa fedha zote za Halmashauri zinakusanywa na halmashauri kwa kutumia mifumo ya kieletroniki.
Kufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha zote za Halmashauri na kuandaa taarifa kwa Afisa Masuuli.
Kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na mali za Halmashauri pamoja na kuhakiki uwepo wa thamani ya fedha.
Kuhakikisha malengo ya halmashari yanafikiwa na kuwa na uwajibikaji.
Kuhakikisha kuwa sheria, kanuni na taratibu za fedha za serikali zinafuatwa kama zilivyo ainishwa kwenye sheria mbalimbali za serikali.
Kupitia majibu ya hoja za ukaguzi zinazojibiwa na wakuu wa idara na kushauri njia sahihi ya kutatua kurekebisha changamoto zinazojitokeza.
Kuangalia na kukagua mifumo ya computer inayotumiwa na Halmashauri na Kutoa ushauri kwa afisa masuuli juu ya ufanisi wake au matatizo yanayoikabali mifumo hiyo na namna ya kukabiliana na changamoto zake.