WAZIRI NAPE AKABIDHI "AMBULANCE" MBILI HOSPITAL YA NYANGAO.
Waziri wa Habari, Mawasaliano na Teknolojia ya Habari na Mbunge wa jimbo la Mtama Mheshiwa Nape M. Nnauye leo tarehe 27 Aprili 2024 amekabidhi magari mawili ya kubebea wagonjwa "ambulance" kwa uongozi wa Hospital ya Nyangao. Hafla hiyo imefanyika Hospital ya Nyangao.
Mheshiwa Nape aliishukuru Serikali ya awumu ya sita chini ya Mheshiwa Rais Daktari Samia Suluhu Hassani kwa kutoa magari hayo kwani ni yataongeza chachu na ufanisi wa huduma za Afya kwa wananchi na Hospitali kwa ujumla akiongeza kuwa kwa miaka mitatu ya Mama Samia Halmashauri ya Mtama imepokea fedha Bilioni 8 kwa ajili ya huduma za afya.
Katika Hafla hiyo Ndugu Dismas Masulubu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama alisema kuwa maboresho ya huduma za afya ndani ya Halmashauri yanadhihilika kwa kupunguza 50% ya vifo vya mama wajawazito, kupungua kwa watoto wanazaliwa chini ya uzito kutoka 11.8% mwaka 2020 hadi 5.8% mwaka 2023 na ongezeko la matumizi ya choo bora kutoka 25% mwaka 2020 hadi 65% mwaka 2023.
Pia Padre Silvanus Kessy kwa niaba ya Askofu wa Jimbo katoliki Lindi aliishukuru Serikali kwa kazi kubwa iliyofanyika ya kuboresha huduma za afya pia aliwakilisha changamoto kama vile ukosefu wa vifaa tiba kama Ventilator na CTC scana, changamoto ya malipo mapya ya bima ya afya na aliongeza kuwa Mamba wa mto Lukuledi ni changamoto kwa jamii ya Nyangao.
Aidha Waziri Nape alipokea changamoto hizo na kuahidi kuzifanyia kazi akisisitiza kuwa atamleta Waziri wa Afya kwa lengo la kumalizia changamoto hizo na aliongeza kuwa Serikali itaangalia namna ya kupunguza mamba mto Lukuledi.
Yote ya yote Mheshiwa Nape alisema Serikali itaendelea kushirikiana na Hospital ya Nyangao, akaendelea akisema Serikali imewekeza sana katika sekta ya Afya na mpango wa Serikali kila mtu awe na bima ya Afya, aliongeza kuwa kutokana na kasi ya maboresho ya huduma za afya anaamini ipo siku wananchi wa Mtama watapata matibabu ya magonjwa yote ndani ya Halmashauri yao, Mwisho alitoa pole kwa wananchi wa nyangao kufuatia mahafa ya mafuriko na Mwanafunzi kuliwa na Mamba.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.