Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Moses Nnauye Kwa niaba ya Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa ameongoza hafla ya Uwasilishwaji na Uhamasishaji wa matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya Mwaka 2022 kwa viongozi, watendaji na wadau wa ngazi mbalimbambali katika Mkoa wa Lindi, Hafla hiyo imefanyika leo tarehe 21 February 2024 ndani ya uwanja wa ILULU uliopo Manispaa ya Lindi.
Akizungumza na wadau wa hafla hiyo Mh. Nape alisema Sensa ya mwaka 2022 imekuwa ya kihistoria kwani ilifanyika sensa ya watu na makazi pamoja na anuwani ya makazi ambapo imepelekea kuwa kivutio kwa nchi jirani, na hayo yote yamefanikiwa kutokana na utashi wa Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Lakini pia Mh. Nape alielezea takwimu za sensa katika mkoa wa Lindi kama ifuatavyo: idadi ya watu katika mkoa wa Lindi iliongezeka kutoka watu 864652 (sensa 2012) hadi watu 1194028 (sensa 2022) sawa na ongezeko la watu 329376 katika kipindi Cha miaka kumi (2012 -2022). Aidha kati ya watu1194028 wanawake ni 611908 na wanaume ni 582120.
Kwa mujibu wa matokeo ya sensa ya watu na makazi ya Mwaka 2022, Halmashauri ya Wilaya ya Mtama ina jumla ya watu 166,493 ambapo idadi ya wanaume ni 79425 na wanawake ni 87068, Halmashauri hii ina jumla ya kaya 50,708 na kata yenye watu wengi ni kata ya kiwalala na kata yenye watu wachache ni kata ya Mtumbya.
Aidha Mh. Nape alikabidhi picha ya ramani inayoonesha idadi ya watu katika Kila kata ndani ya Halmashauri, picha hizo zilipokelewa na wakurugenzi wa Halmashauri husika. Mwisho hafla hiyo iliudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali kama vile spika wa bunge mstaafu mama Anna Makinda, Mkuu wa mkoa wa Lindi, katibu Tawala mkoa Lindi, wakuu wa Wilaya, madiwani, viongozi wa dini, viongozi wa chama Cha mapinduzi na wajumbe mbalimbali.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.