Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga kwenye hotuba yake tarehe 15, Januari, 2022 alipokuwa katika sherehe maalumu ya kuaga mwaka 2021 na kukaribisha mwaka 2022 iliyofanyika katika Kata ya Nyangao ambapo amesema kuwa ili kuhakikisha Halmashauri ya Mtama inakuwa na mabadiliko ya kimaendeleo ni lazima watumishi waongeze kasi ya kiutendaji hususani katika usimamiaji na utekelezaji wa majukumu yao.
Aidha Ndemanga amewataka Madiwani kufanya kazi kwa ushirikiano kwenye Kata zao huku akiwaomba Wakurugenzi kutoka Wilaya nyingine walioalikwa kwenye sherehe hiyo kufanya kazi kwa pamoja ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu wa kiutendaji na kwamba kwa kufanya hivyo kutasaidia kuinua kiwango cha maendeleo Mkoa wa Lindi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndg. George Mbilinyi alimshukuru Mungu kwa kuvuka salama 2021 lakini pia amemshukuru Rais wa awamu ya sita Mhe. Samia Suluhu Hassani kwa kupeleka fedha Tsh Bill.19 kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo sekta ya afya, elimu, maji pamoja na barabara. Aidha alichukua fursa hiyo kumpongeza Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye kwa kupata uteuzi huo lakini pia amekuwa chachu ya kusukuma maendeleo katika Halmashauri hiyo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hassani Ngoma alipata nafasi ya kutoa salamu za mwaka mpya ambapo alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Mtama kwa kuandaa tukio hilo huku akiahidi kutoa ushirikiano na Wilaya ya Lindi katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo.
Sherehe hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi ambaye alikuwa Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Nachingwea, Ruangwa, pamoja na Manispaa ya Lindi. Lakini pia wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo za Benki ikiwemo NMB, CRDB.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.