Rai hiyo imetolewa tarehe 23/09/2021 na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndg. Mahmoud Kimbokota alipofanya Ziara ya kikazi katika kituo cha afya Nyangamara akiambatana na Wataalam wa Idara mbalimbali wa Halmashauri hiyo.
Akizungumza na watumishi wa kituo hicho Kimbokota amewataka watumishi hao kutimiza wajibu wao kiutendaji kazi ikiwa ni pamoja na utoaji wa huduma bora kwa Wananchi huku akisisitiza uhamasishaji kwa wananchi juu ya uelewa kuhusu uchangiaji wa huduma za afya pamoja na uwepo wa Mifumo ya taarifa na ukusanyaji wa Mapato (GoT-HOMIS). Aidha Kimbokota amewataka viongozi ngazi ya Kijiji kuendelea kutoa hamasa kwa wananchi wajitokeze kwa wingi kufanya usafi katika maeneo yao pamoja na maeneo ya kituo cha afya ili kuwa na mazingira safi na salama kwa watoa huduma pamoja na wagonjwa.
Kwa pande wake Mganga Mfawidhi wa kituo hicho Dkt. Joel Msilimu akitoa taarifa fupi ya kituo amesema pamoja na mafanikio mbalimbali yaliyopo kituoni hapo bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa watumishi ambapo kwa sasa wana jumla ya watumishi 13 tu, huku akieleza kuwa suala la kukatikakatika kwa umeme limekuwa ni kikwazo kinachorudisha nyuma kasi ya utendaji kazi lakini pia hupelekea baadhi ya vifaa kuharibika na kusababisha hasara kwa kituo.
Katika ziara hiyo, wametembelea jengo la wazazi, jengo la upasuaji, jengo la maabara pamoja na jengo la kuhifadhia dawa.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.