Mafunzo hayo yametolewa Julai 13, 2021 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama na kufunguliwa na mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndg. Samwel Gunzar .
Mafunzo hayo yamehudhuriwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Lindi NdG. Thomas Safari, baadhi ya wakuu wa idara wa Halmashauri ya Mtama, Maafisa Tarafa, Watendaji wa kata na Watendaji wa serikali za vijiji, kwa lengo la kujenga uelewa zaidi juu sera na sharia za ardhi, haki za kumiliki ardhi pamaoja na namna bora ya kukabiliana na changamoto na utatuzi wa migogoro mbalimbali inayojitokeza katika jamii.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Lindi NdG. Thomas Safari, ametoa wito kwa washiriki wa mafunzo hayo kuhakikisha wanakua mabalozi wazuri kwa kusaidia kutoa elimu hasa katika ngazi za shule za msingi na jamii kwa ujumla kuhusu athari za ubaguzi katika umilikaji wa ardhi ili kukuza kizazi kitakachokuwa na uelewa zaidi kuhusu sera na sharia za ardhi. Pia amewataka washiriki kufanya kazi kwa njia ya ushirikishwaji.
Nae Afisa Tarafa ya Nyangamara Ndugu Hezron Meshack Elias alipata nafasi ya kuchangia juu ya suala la umiliki wa ardhi kwa vijana na kusema kuwa kwa upande wa vijana wana nafasi kubwa ya umiliki wa ardhi lakini bado kuna changamoto kwa vijana kutojihusisha na kilimo hali inayopelekea kutozithamini ardhi wanazomiliki. Pia ametoa ushauri kwa washiriki kujikita zaidi katika kuhamasisha vijana kujihusisha na kilimo ili vijana hao wafahamu umuhimu wa ardhi kimaendeleo.
Mwezeshaji wa Mafunzo hayo kutoka chuo kikuu cha Ardhi Dkt. Fredrick Bwire Magina, ametoa wito kwa wasuluhishaji wa migogoro ya ardhi kutojihususha na vitendo vya Rushwa wakati wa utekelezaji wa majukumu yao na kuongeza watatuzi wa migogoro hiyo wanatakiwa kufika eneo la tukio ili wajiridhishe na ushahidi wa wahusika.
Katika mafunzo hayo, washiriki walipata nafasi ya kuuliza maswali na kujadili kwa pamoja mada zilizowasilishwa na wawezeshaji wa mafunzo hayo huku baadhi yao wakitoa changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao hususani suala la uwepo wa migogoro ya ardhi katika maeneo yao na kupatiwa ufumbuzi wa namna ya kutatua changamoto hizo.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.