Wananchi kutoka katika kona mbalimbali za Wilaya ya Lindi na viunga vyake wamefurika kwa wingi kuhudhuria mnada wa kihistoria uliofanyika katika Kata ya Kitomanga iliyopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, Mnada huo wa Mwanzo ambao uliweza kuwakusanya baadhi ya Wafanyabiashara,Wananchi na Wauzaji wa Mifugo kutoka katika kata za Kilangala na kitomanga waliweza kuleta Mifugo yao hasa Ng'ombe na Vyombo vya Majumbani , Ng'ombe wapatao 21 waliweza kununuliwa katika mnada huo.
Mnada huo hufanyika katika Kata ya Kitomanga na mara mbili yaani kila tarehe 15 ya kila mwezi na 30 ya Mwisho wa Mwezi na Mnada huo unawahusisha Mifugo na vitu vingine vya Majumbani. Mnada huo uliweza kuiingizaia Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya Ushuru mana kila Ng'ombe mmoja hutozwa kiasi cha shilingi 3,000/= hivyo kufanya kuingiza kiasi cha shilingi 63,000/= katika mnada huo
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.