Elimu ya Usafi wa mazingira imetolewa tarehe 19-20 Julai 2021 kwa njia ya uchefushaji (COMMUNITY LED-TOTAL SANITATION) katika Kijiji cha Mahiwa Kata ya Nyangao na Muungano Kata ya Namupa ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mtamaa kwa lengo la kubadilisha tabia za wananchi kujisaidia hovyo hali inayopelekea uchafuzi wa mazingira katika maeneo yao yanayowazunguka na badala yake wajenge vyoo ili waishi katika mazingira safi na salama.
Kupitia Mpango wa maji safi vijijini WASH kutoka Shirika la World Vision Diocese ya Masasi imeratibu zoezi zima kwa kushirikiana na idara ya afya Halmashauri ya Wilaya ya Mtama na kufanikiwa kuvifikia takribani vijiji viwili Mahiwa kata ya Nyangao pamoja na Muungano kata ya Namupa ambapo jumla ya wanachi 314 wamefikiwa na elimu hiyo.
Kutokana na elimu hiyo kupitia zoezi la uchefushaji wananchi wa vijiji hivyo wamejiwekea mikakati na maakubaliano ya ujenzi wa vyoo ifikapo Agosti 20 2021.
Uchefushaji ni njia mojawapo ya kuwafanya wananchi kuacha kujisaidia ovyo katika maeneo yao na kuwafanya wajenge vyoo ambapo njia hii huwafanya wananchi kuona aibu, uoga,kukereka na kutoridhika na kupelekea watu kutambua uchafu walionao ili waweze kuacha uchafuzi wa mazingira na kuishi katika mazingira safi na salama.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.