Ni matamanio ya muda mrefu ya uhitaji wa kituo cha Afya Kata ya Mtama yaliyowasukuma wananchi wa Kata ya Mtama wakishirikiana na uongozi wa Halmashauri chini ya usimamizi wa Mkurugenzi Ndg. George Emmanuel Mbilinyi kujitokeza kwa wingi kushiriki kwa pamoja kusafisha eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya cha Kata. Wananchi hao wametoa wito kwa jamii nzima ya Mtama kujitokeza kwa wingi kusafisha eneo hilo kwani kwa kufanya hivyo ni kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuleta maendeleo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndg. George Emmanuel Mbilinyi ametoa shukurani kwa Rais wa awamu ya sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho. Aidha amewataka wananchi waliojitokeza kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu lakini pia waendelee kuwekeza nguvu zao kwa lengo la kukamilisha kwa haraka mradi huo.
Jumla ya shilingi Milioni 250 tayari zimetolewa kwa awamu ya kwanza zitakazojenga majengo matatu la OPD, Maabara pamoja na kichomea taka ujenzi wa kituo hicho unatarajiwa kuanza tarehe 11 Octoba 2021.
Kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho kutawapunguza wananchi wa Mtama na maeneo jirani changamoto ya kusafiri kwa umbali mrefu kufuata huduma za afya.
Mkurugenzi akizungumza na wananchi waliojitokeza kufanya usafi
mwananchi akikata mkorosho
muweka hazina wa Halmashauri pia alishiriki
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.