Wananchi wa Kijiji cha Chiwerere Kata ya Namangale Januari 19, 2022 wameupokea kwa matumaini na furaha Mradi wa umaliziaji wa zahanati iliyojengwa kwa nguvu na michango ya wanajamii na kutoa shukurani kwa Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan
Wananchi hao wameahidi kuendelea kujitolea katika shughuli zote za umaliziaji ikiwa ni pamoja na kupeleka mchanga, mawe pamoja na mbao zitakazopatikana kupitia msitu wa hifadhi wa kijiji hicho. Aidha wananchi hao wamesema kuwa kukamilika kwa ujenzi huo kutarahisisha upatikanaji wa huduma za afya hususani kwa wanawake wajawazito pamoja na wazee.
Waliongeza kuwa wameamua kujitolea hadi kufikia hatua ya boma lenye kozi 11 kutokana na hadha na gharama wanazozitumia kufuata huduma za afya katika hospitali ya Nyangao na kwamba kwakua Serikali imeziona jitihada za wananchi wa Chiwerere basi wako tayari kuunga mkono kwa kuendelea kujitolea.
Awali ya hapo Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya Ndg. Mfaume Hemed ambaye ni Afisa Afya aliwapongeza wananchi hao kwa ushirikiano na juhudi walizozitoa katika ujenzi huo. Sambamba na hilo Mfaume aliendelea kwa kusema kuwa Serikali imeunga mkono jitihada hizo kwa kupeleka fedha Tshs. Milioni 50 ili kuweza kumalizia zahanati hiyo.
Aidha amewaomba viongozi wa kijiji hicho kuhakikisha wanabainisha mipaka ya eneo la mradi huo lakini pia kuangalia njia bora ya kuongeza eneo ili kuwa na nafasi ya kuongeza majengo mengine ikiwa ni pamoja na nyumba za watumishi.
Kwa upande wake Mtendaji wa Kijiji hicho Hamisi Mtioli amewasihi wananchi kuondoa dhana ya kupatikana kwa fedha hizo ndio mwisho wa kujitolea badala yake waendeleze umoja na mshikamano wakati wa umaliziaji wa mradi huo.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.