Wananchi wa Kijiji cha Namupa na Muungano Kata ya Namupa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Mkoani Lindi wametakiwa kuzingatia vigezo na kanuni zilizotumika wakati wa kuzitambua kaya masikini kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya masikini (TASAF).
Rai hilo limetolewa tarehe 12/11/2021 na Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mtama Bi. Sharifa Tapalu alipokuwa akitoa majibu ya maswali yaliyoulizwa na wananchi wa Vijiji hivyo walipohoji kwanini wazee wameachwa na kuchukuliwa vijana wenye nguvu za kufanya kazi zao na kuwa walengwa kwenye mpango huo.
Kabla ya kutoa ufafanuzi wa swali hilo Bi. Sharifa alianza kueleza dhumuni la Mradi wa TASAF ambapo amesema lengo kuu ni kunusuru kaya masikini na kuleta mabadiliko chanya katika jamii. Alisema kuwa watu wengi wanaamini kuwa TASAF ni kwa ajili ya wazee na kuwataka wafahamu vigezo vinavyotumika wakati wa utambuzi wa kaya hizo.Aliongezea kusema kuwa kaya wanazozilalamikia zilitambuliwa na wananchi wenyewe kupitia mikutano ya hadhara ikiwa ni hatua za awali za zoezi la kuibua mradi huo.
Alivitaja vigezo hivyo ikiwa ni pamoja na:
Mkutano huo uliongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mtama Ndg. Mahmoud Kimbokota katika kijiji cha Namupa kwa lengo la kuhamasisha wananchi wa vijiji hivyo kuendelea kujitolea kufukia mitaro ya maji mradi wa Namupa-Mahiwa unaofadhiriwa na Kanisa la Anglikana pamoja na kusikiliza kero za wananchi.
Awali ya hapo, mjadiliano mzito uliendelea mkutanoni hapo kujadili suala la Wananchi hao kuonekana kutokubali kuendelea kujitolea kwenye mradi huo ambapo walipata nafasi ya kutoa sababu zao ikiwa ni pamoja na kukosa ushirikishwaji wa viingozi kwenye utekelezaji, wataalamu kuzuia kufukia ili kupisha uwekaji wa vituo vya kupumzikia maji, uchache wa vilula vya maji.
Mwanchi akitoa hoja
Afisa Utumishi akiongoza mjadala
Kufuatia majadiliano hayo, Kaimu Mkurugenzi ambaye ni Afisa Utumishi Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Mahmoud Kimbokota aliwataka wananchi hao kuweka pembeni tofauti zao na waendelee kujitolea na kwamba wananchi hao walikubaliana kuendelea na shughuli ya ufukiaji wa bomba la maji. Aidha , Kimbokota aliwaelekeza watumishi na wataalamu mbalimbali kufanya kazi kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo wa hali ya juu ili kutoa huduma bora katika jamii.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.