Wanafunzi hao wamenufaika kupitia Programu iliyoanzishwa Mwezi Julai chini ya uratibu wa Mama Rhobi Nnauye mke wa Mbunge wa Jimbo la Mtama kwa niaba ya Mh. Nape Moses Nnauye Mbunge wa jimbo hilo kwa lengo la kupunguza changamoto zinazowakabili wanafunzi wa kike na kuongeza Ari na kujiamini katika kipindi kizima cha maandalizi ya mitihani yao ya kidato cha nne.
Mama Rhobi Nnauye amekamilisha zoezi la ugawaji wa taulo za kike tarehe 29 Julai 2021 katika shule za sekondari kata ya Nyangamara na Mandwanga ndani ya Halmashauri hiyo akiambatana na wenyeji wake Diwani viti Maalumu kata ya Nyangamara Mh Asha Nguli, Mwenyekiti wa UWT kata ya Nyangamara Bi. Zainabu Madevu na Makamu mwenyekiti Bodi ya kituo cha Afya Nyangamara na kufanikiwa kutoa jumla ya taulo 118 kwa wanafunzi zaidi ya 64 katika shule ya sekondari Nahukahuka, Mandwanga, Chiuta, Mbawe na Litipu kwa wanafunzi wa kike kwa kidato cha nne.
Katika zoezi hilo Mama Rhobi Nnauye alipata nafasi ya kuzungumza na wakuu wa shule na baadhi ya walimu walezi ili kubaini changamoto za kiutendaji ambapo wengi wao wamezungumza kuhusiana na suala la muhamko mdogo wa wazazi juu ya elimu kwa watoto wao jambo ambalo linapelekea kurudisha nyuma jitihada za walimu na wanafunzi hao kufanya vizuri katika masomo yao pia wametoa shukurani zao kwa msaada wa taulo hizo kwanini zitapunguza ongezeko la utoro shuleni. Aidha Mama Rhobi Nnauye alipata nafasi ya kuzungumza na wanafunzi wa kike wa kidato cha nne ambapo amewataka wanafunzi hao kutochanganya mapenzi na masomo pia amesisitiza zaidi ushirikiano baina yao na kusaidiana katika masomo ili kufikia malengo yao. " Najua kila mtu ana malengo yake lakini hatuwezi kufikia malengo Hayo bila ushirikiano, niwasihi sana msichanganye mambo yasiyohusiana na masomo mnachotakiwa ni kupambania ndoto zenu na kila kitu kinawezekana." Rhobi Nnauye.
Kwa upande wa diwani viti maalumu kata ya Nyangamara ametoa shukurani kwa Mama Rhobi kwa kuoneshwa kuwajali watoto wa kike lakini pia amewahasa wanafunzi kuyasikiliza yaliyozungumzwa na mgeni rasmi huku akitoa msisitizo zaidi kuhusu kusoma kwa bidii ili kufikia malengo yao.
Zoezi lilianza Julai 2021 na Mpaka sasa amefanikiwa kugawa taulo za kike zaidi ya 1,300 kwa wanafunzi wa kike wa kidato cha nne 564, kwenye sekondari 17 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama huku akiwa na matarajio ya kugawa taulo za kike 3,000 ndani ya Halmashauri hiyo.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.