'Elimu haina Mwisho', 'Elimu ni ufunguo wa Maisha' ni miongoni mwa Misemo iliyopo katika maisha yetu ya kawaida yote ikiwa na lengo kuu la kutafuta elimu mahali popote na sehemu yeyote haya yamedhihilika mara baada ya Walimu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Lindi kuamua kwa ridhaa yao wenyewe kwenda kufanya ziara ya kujifunza Mkoani Mwanza na kutembelea Halmashauri ya Jiji la Mwanza la Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela. Lengo kuu ni kujua hasa siri iliyopo katika Halmashauri hizi ni kwanini zinafanya vizuri Kitaaluma katika ufaulishaji wa Wanafunzi, kwani kwa Upande wa Halmashauri ya jiji la Mwanza Mwaka 2017 ilifaulisha kwa asilimia 88.7 na 2018 kwa asilimia 92..3 na Mwaka 2019 imejiwekea lengo la kufaulisha kwa asilimia 100 ikiwa na mana hakuna mwanafunzi atakayshindwa kuingia kidato cha kwanza, na katika upande wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mwaka 2017 asilimia 87.5 na mwaka 2018 ni asilimia 94.8 na mwaka 2019 wana lengo la kufikisha asilimia 100 wakati Halmashauri ya Wilaya ya Lindi kwa Mwaka 2017 ilifaulisha kwa asilimia 65.1 na mwaka 2018 ilifaulisha kwa asilimia 61.
Hapo ndiyo utaona kwa nini Halmashauri ya wilaya ya Lindi ikaenda kufanya ziara hii ya Kikazi na kuamua kuzitembelea Halmashauri hizi mbili lakini mara baada ya kujifunza kutoka katika Halmashauri hizi mbili Walimu wa Halmashauri ya Lindi walifanikiwa kutoka na mambo haya Mosi,Wana walimu wa kutosha na uwiano mzuri kwa mwalimu na Wanafunzi Pili,Wanamiundombinu mizuri hususani Vyumba vya Madarasa Tatu,Ushirikiano wa kutosha kwa ngazi zote za utawala Nne,Walimu kuwa na Moyo wa Uzalendo wa kufundisha hata kwa muda wa ziada na Likizo bila malipo yeyote Tano,Walimu Kutatuliwa kero zao za likizo na uhamisho kwa wakati na kurekebishiwa madaraja yao Sita,kuwa na mpango kazi unaotekelezeka Saba,Walimu kumaliza mada husika kwa mujibu wa mtaala(syllabus) Saba,Wanasiaasa kuwa ni sehemu ya wasimamizi wa wa mipango ya Elimu Nane,Kudhibiti utoro wa walimu na wanafunzi Tisa,Ufuatiliaji wa karibu wa Hali ya ufundishaji na ujifunzaji mashuleni kumi,Kuwahusisha wadau changamoto zote za kielimu na kutafuta ufumbuzi kwa pamoja.
Baada ya kujifunza mazuri haya kutoka kwa wenzetu walimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi walipata fursa ya kwenda kuona vivutio mbalimbali vilivyopo jiji la mwanza kama visiwa vya saa 8,jengo la Rock city na Bandari kuu ya Mwanza
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.