Wakazi wa kijiji cha Mikongi iliyopo kata ya Mandwanga,Halmashauri ya wilaya ya Lindi wamekutwa na butwaa baada ya kuvamiwa na watu zaidi ya 50 kutoka kijiji cha Nambau wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara kutokana na imani za kishirikina, kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi ya wilaya ya Lindi ambaye ni Mkuu wa Wilaya Ndg Shaibu Ndemanga alisema kwamba uharifu huo uliofanywa na watu takribani ya 50 ambao walitoka katika katika kijiji cha Nambahu,Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara waliokwenda Mikongi kwa lengo la kusaidia kumtafuta mtoto wa miaka tisa Farida Hasani aliyekuwa anasoma darasa la Tatu katika shule ya Msingi ya Nambahu iliyopo Tandahimba na akapotea katika kijiji cha Mikongi alipokwenda kumtembelea bibi yake.
Ndemanga alisema mtoto huyo aliweza kupatikana akiwa hai alitoweka tarehe 08/06/2018 asubuhi kutoka nyumbani kwa bibi yake ambapo juhudi za kumtafuta hazikuweza kuzaa matunda kuanzia tarehe hiyo hadi tarehe 10 mwezi huu alipoonekana, naye Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Mikongi ndg Juma Likomboleka aliema tarehe 09.06.2018 watu zaidi ya 50 waliweza kuvamia kijiji chake kwa kutumia usafili wa gari na pikipiki za tairi tatu maarufu kama Guta kwa lengo la kusaidia kumtafuta mtoto huyo ambaye ni mkazi mwezao wa kijiji cha Nambahu.
Mwenyekiti huyo wa kijiji alieleza kuwa ilipofika majira ya saa nane usiku vijana watano kati yao waliondoka na kuelekea madukani wakiwa wamebeba mapanga,hata hivyo waliweza kutiwa nguvuni na migambo na kufungiwa ofisini hata hivyo kaimu Mtendaji Kata aliwafungulia vijana hao usiku huo huo, kwa upande wa Farida Muanya ambaye ndiye bibi wa mtoto huyo alisema siku ya Tarehe 10/06/2018 mchana watu hao wakiwa wameongozana na Baba wa mtoto huyo walimtishia maisha Mume wake Shaibu Kazumari kwa kumtuhumu kuwa ndiye aliyemficha mtoto huyo ili amfanye msukule na kwamba asipoonekana basi wangemzuru ndipo mzee huyo akaamua kutoloka kijijini hapo.
Bi Maunya aliendelea kueleza kuwa Mzee Shaibu baada ya kukimbia kutoka nyumbani kwake kwa kuhofia uhai wake ndipo vijana hao walianza kufanya vurugu na uharibifu wa mali ikiwemo kubomoa nyumba mbiliza bati na kucoma moto nyumba moja ya nyasi,jiko na kuchoma moto Pikipiki na kuharibu vibaya kisima cha maji,kwa upande wake Kamanda wa polisi mkoa wa lindi Kamishina msaidizi wa jeshi la polisi(ACP) pudesiana Protaz amethibisha kuwepo kwa tukio hilo na kusema kuwa watu watano akiwemo Kaimu afisa mtendaji wa kata ya Mandwanga,Abdallah Mkondela wamekamatwa na polisi kuhusiana na tukio hilo. pia lisema jeshi la polisi linamshikilia mwatu mmoja ambaye alipatikana na mtoto huyo na ambaye ametambulika kwa jina la Hamis Mmalunda pia jeshi la polisi linaendeleza kuwatafuta wazazi wa mtoto baada ya kutekeleza uharifu huo walipotea kusikojulikana.
kamanda prostas alisema kuwa uchunguzi wa awali hauoneshi kutoweka kwa mtoto huyo hakukuwa na mazingira yeyote ya ushirikina na Mwishowe aliwaasa wananchi kutojichukulia sheria mikononi na huku akiahidi kuwakamata wahusika wote waliofanya uhalifu huo.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.