Maadhimisho ya Sherehe ya Wafanyakazi duniani yanafanyika kila Mwaka ifikapo Mei Mosi na ikiwa na lengo la kuwakutanisha Wafanyakazi wote kutoka taasisi zote za Serikali na za Binafsi ili kwa pamoja wazweze kutoa Changamoto zao zinazowakabili kwa Mwajiri na Serikali kwa ujumla ili ziweze kutatuliwa, Maadhimisho ya Mwaka huu kitaifa yalifanyika katika Mkoa wa Iringa na Mgeni rasmi alikuwa ni Raisi wa Jamhuri ya Tanzania
Katika Mkoa wa Lindi Maadhimisho ya Sherehe ya Wafanyakazi yalifanyika katika Wilaya ya Lindi katika Kiwanja cha Bustani ya Mkapa(Mkapa Garden) ambapo Mgeni rasmi katika Hafra hii alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi ambaye alizungumza mambo mengi ya kiutumishi ikiwa ni pamoja na kuwataka watumishi kufanya kazi kiufanisi kwani Mhe Rais bado anaendeleza juhudi zake za kumfanya Mtumishi aishi Maisha mazuri ikiwa ni pamoja na Kumlipa stahiki za Uhamisho mara tu anapohama na sio kucheleweshwa, watumishi wote ambao bado wanaidai Serikali kulipwa Fedha zao mara moja na anapohama
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Gofrey Zambi aliwataka Maafisa Watumishi wote kuendelea kuhakiki taarifa za Watumishi mana Bado Watumishi Hewa bado wapo na pia alisisitiza, Pia aliendelea kusisitiza Maagizo yWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Mkuchika (Mb) kuhusiana na Uhamiso wa watumishi na kuwataka Waajiri kuwapitishia Barua watumishi wao mara wanapotaka kuhama kutokana na sababu Mbalimbali na kuwasisistiza kuwa wao siyo wa Mwisho kufanya Maamuzi mana mtu anayeandikiwa kufanya ni katibu mkuu wa Utumishi na kuwasisistiza Wakurugenzi kupitisha Barua hizo ila kama ana upungufu wa watumishi wa kada hiyo anayohama anaweza kumpitishia lakini akatoa angalizo kama kuna upungufu wa watumishi
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.