Ushauri huo wenye msisitizo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndg. George Emmanuel Mbilinyi tarehe 3/11/2021 alipokutana nao katika kikao cha wafanya biashara hao kwenye Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri kilicholenga kutambulisha miradi mbalimbali ya maendeleo na kuangalia namna ya kufanya kazi kwa pamoja.
Kikao hicho kilihudhuriwa na baadhi wawakilishi wa wafanya biashara ambao wanajishughulisha na uuzaji wa vifaa vya ujenzi pamoja na chakula.
Mkurugenzi alisema kuwa Serikali ya awamu ya sita imeleta fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vituo vya afya, nyumba za watumishi ikijumuisha nyumba ya Mkurugenzi lakini pia ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na vyoo katika shule za Msingi na Sekondari. Sambamba na hilo Ndg. Mbilinyi alitoa msisitizo kwa wafanya biashara hao kujisajili katika Mfumo wa Wakala wa Manunuzi ya Serikali ili kuwa na sifa ya kufanya kazi na kutambulika sehemu yeyote yenye fursa za kibiashara pamoja na kuunda chama au umoja ili kurahisisha mawasiliao ya kibiashara kupitia viongozi wao.
Amewaomba kutopanga bei kwa maslahi yao binafsi na badala yake wanatakiwa kuwa na bei rafiki katika huduma zao ili kuishawishi Halmashauri kutoa kipaumbele kwa wafanya biashara hao kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia hali ya mzunguko wa fedha kubaki ndani ya mji wa Mtama lakini pia watakuwa ni sehemu ya watu walioijenga Halmashauri hiyo. Aidha, Mkurugenzi huyo hakusita kuendelea kuhamasisha uchangiaji wa mapato kwa kulipa ushuru kulingana na ukubwa na aina ya biashara zao. Aliwasisitizia kuwa wao kama wafanya biashara wanatakiwa kuchangia mapato ya Halmashauri na kwamba namna bora ya kuiendeleza ni ulipaji ushuru.
Kwa upande wake Mfanya biashara ya usambazaji wa vifaa vya ujenzi Bw. Mchora Selemani alipata nafasi ya kutoa changamoto wanazokutana nazo pindi wanapofanya kazi na Halmashauri ikiwa ni pamoja na ucheleweshwaji wa malipo hali inayopelekea malimbikizo makubwa ya madeni. Kufuatia hoja hiyo, Mkurugenzi amewaahidi kuwa watalifanyia kazi na kuanzia sasa mdau yeyote atakayefanya kazi na Halmashauri malipo yake yatafanyika kwa wakati kulingana na makubaliano yaliyofikiwa. Mwisho aliomba kuwa na ushirikiano wa pamoja.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.