Mafunzo hayo yametolewa tarehe 7 Oktoba 2024 katika kambi tatu(3) tofauti ambazo ni ukumbi wa Shule ya Sekondari Nyangao, ukumbi wa HeinBeck uliopo kata ya Nyangao pamoja na ukumbi wa Mtama Break Point uliopo kata ya Mtama huku Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo zaidi waandikishaji hao.
Aidha zoezi la uandikishaji litaanza siku 47 kabla ya siku ya Uchaguzi ambapo litafanyika Kwa siku 10 mfululizo kuanzia tarehe 11 Oktoba hadi tarehe 20 Oktoba 2024, lakini pia vituo vya uandikishaji vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 Asubuhi hadi saa 12:00 jioni.
Hata hivyo, Bi: Emma Lunojo Mwezeshaji wa mafunzo hayo amewataka waandikishaji hao kuwasisitiza Wananchi wenye sifa kujitokeza Kwa wingi kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura katika Kitongoji husika kwani watakao jiandikisha ndio watakao piga kura Novemba 27 Mwaka huu.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.