Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey W. Zambi, amezindua rasmi zoezi la utoaji wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi, leo hii, kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 Katika sherehe iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Lindi.
Miongoni wa waliohudhuria walikua ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Lindi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Lindi, katibu tawala wa Wilaya pamoja na katibu tawala wa Mkoa. Wengine waliohudhuria ni watumishi mbali mbali na wanafunzi ambao pia walipatiwa chanjo katika uzinduzi huo.
Wakizungumza katika nyakati tofauti tofauti katika uzinduzi huo Mstahiki Meya wa Manispaa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi waliwaasa wanafunzi hao kuwa kupewa chanjo hii haina maana kuwa wamepewa ruhusa yakufanya yale ambayo wamekatazwa.
Aidha mkuu wa mkoa katika kukazia hilo alisema kuwa hawapaswi kujihusisha na vitendo vya ngono maana madhara yake ni makubwa “madhara ya ngono ni makubwa, kuna ukimwi pamoja na mimba. Na chanjo hii ni kwa ajili ya saratani ya mlango wa kizazi na si hayo mengine”
Pia wanafunzi wliohudhuria uzinduzi huo waliombwa kwenda kuwa mabolizi wazuri kwa wenzao juu ya zoezi hili linaloendelea.
Zoezi hilo ambalo lilikuwa limeshaanza siku tano zilizopita, leo lilikuwa linazinduliwa rasmi. Zoezi hilo ambalo limefadhiliwa na WHO limewalenga mabinti wa kuanzia miaka 9 hadi 14, Japo chanjo imeanza kwa kutolewa kwa masichana wenye miaka 14
Mratibu wa zoezi hilo alisema “hii sio kampeni bali ni zoezi endelevu”.
Saratani ya mlango wa kizazi ni ugonjwa hatari na unaouwa wanawake wengi hasa katika nchi zinazoendelea kama Tanzania. Ugonjwa huu unasababishwa na vijidudu vijulikanavyo kitaalamu kwa jina la Human papilloma virus (HPV) na huambukizwa kwa njia ya ngono kutoka kwa mtu mwenye virusi hivyo. Tafiti zinaonyesha kuwa katika kila wanawake wanne wanaoshiriki ngono watatu wanapata maambukizi ya HPV na kwa wasichana wenye umri mdogo uwezekano wa kupata maambukizi hayo ni mkubwa zaidi.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.