Uongozi wa timu ya mpira wa miguu MTAMA BOYS FC ambayo imechukua ubingwa wa Ligi Daraja la tatu Mkoa wa Lindi tarehe 07 January, 2022 umekabidhi kombe kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mtama Ndg. George Mbilinyi ambaye ni mlezi wa michezo katika Halmashauri hiyo. Hatua hii ni moja ya kuonesha thamani pamoja na kutambua mchango wa viongozi wa michezo na kuwapa matumaini ya kutoa ushirikiano.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa kombe hilo limeiheshimisha Halmashauri na kuahidi kutoa ushirikiano sio tu kwa timu ya Mtama boys bali kwa timu zote za Halmashauri zilizokuwa na utayari katika michezo.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.