Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndugu George E Mbilinyi leo tarehe 6 machi 2024 ameongozana na kamati ya maafa kwa lengo la kutembelea nyumba zilizoathiriwa na mvua katika kata ya Nyangao, Katika kata hiyo nyumba 14 zimebomoka huku nyumba 10 zikibomolewa na wananchi kwa tahadhari.
Athari hizo zimetokana na mto Lukuledi unaopita katika kata hiyo, kutokana na mvua kubwa zinazoendelea ndani ya Halmashauri na maeneo ya karibu mto huo umejaa maji sana na kupelekea kuacha njia yake na kuelekea kwenye makazi ya watu yaliyo karibu mto huo.
Akizungumza na wananchi Mkurugenzi alisema kuwa taarifa ya maafa wameipokea kwa masikitiko makubwa, lakini pia Serikali bado ipo pamoja na waathirika wote wa maafa hayo. Hata hivyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndugu Yusufu Tipu aliongeza kuwa Halmashauri imeunda tume ya maafa ambayo inaendelea kufanya kazi ili kupata tathmini halisi ya watu walioathirika.
Aidha Afisa mazingira wa Halmashauri alitoa ushauri kwa wananchi kuhakikisha wanajenga mita 60 kutoka kwenye chanzo Cha mto na kuachana na shughuli ambazo ni hatarishi kwa mto kama vile uchimbaji wa mchanga.Mwisho wananchi waliishukuru Serikali na uongozi wa Halmashauri kwa kuwatembelea , kuwapa moyo na ushauri katika kipindi hiki kigumu wanachopitia.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.