Hayo yamesemwa na Mh. George Mbilinyi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama leo alipokutana kwa mara ya kwanza na watumishi wa Halmashauri hiyo kwenye kikao cha utambulisho kilichofanyika leo tarehe 11 Agosti 2021 katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Katika kikao hiko Mh. Mbilinyi alipata nafasi ya kujitambulisha na kuwatambua baadhi ya watumishi waliohudhuria. Aidha katika hotuba yake ya kwanza ya utambulishp mara baada ya kuripoti katika kituo chake kipya cha kazi , Mh. Mbilinyi amewataka watumishi wote wa halmashauri kufanya kazi kwa bidii, kwa ushirikiano, kuwa na mahusiano mazuri mahali pa kazi, uwajibikaji, kuwa na nidhamu,pamoja na uzalendo ili kufikia malengo na kuleta maendeleo ndani ya halmashsuri. “ tutaweza kufikia malengo kama tutakuwa na nidhamu, nidhamu katika muda wa kazi, lazima tuheshimu muda wa kazi, lakini ikibidi unajitolea muda wa ziada”Mh George Mbilinyi. Sambamba na hayo Mh. Mbilinyi amewaomba watumishi kumpa ushirikiano wa kutosha ili kuiwezesha Halmashauri ya Wilaya ya Mtama kuwa bora na ya mfano
Nae afisa utumishi wa wilaya Ndg. Mahmoud Kimbokota alipata nafasi ya kusoma historia fupi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mtama na kutoa neno la ukaribisho kwa Mh. Goerge Mbilinyi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.