TIMU YA URATIBU WA MWENGE MKOA YATEMBELEA MIRADI HALMASHAURI YA MTAMA.
Timu hiyo ikiongozwa na Mratibu wa mwenge,katibu Tawala Wilaya ya Lindi, Afisa mipango, Afisa michezo, RUWASA na TARURA, kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Lindi pamoja na wataalamu wa Halmashauri ya Mtama leo tarehe 27 Aprili 2024 wametembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotarajiwa kutembelewa na mwenge wa uhuru mwaka huu ili kujiridhisha na maendeleo ya miradi hiyo.
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni Eneo la kupokelea mwenge Nyangao, kaRakana ya kikundi cha vijana Nyangao, kituo cha redio Mtama, Zahanati Nahukahuka, Madarasa 3, ujenzi wa bwawa la samaki, utunzaji wa mazingira shule ya msingi Songa Mbele pamoja na muendelezo wa barabara ya Nyengedi-Rondo.
Aidha Bi Shekalage Makalage mratibu wa mwenge Mkoa wa Lindi alisema kuwa miradi yote inaridhisha kwa hatua iliyofikia hivyo basi viongozi wanapaswa kufanya marekebisho machache yaliyobakia kwa utaalamu zaidi ili kuendana na kasi ya muda uliobakia kufikia siku ya mapokezi ya mwenge, ambapo Halmashauri ya Mtama inatarajia kuupokea mwenge wa uhuru tarehe 27 Mei 2024.
Lakini pia Bwana Hudhaifa Kassim Rashid Katibu Tawala Wilaya ya Lindi amesisitiza hamasa zaidi kutolewa kwa wananchi ili kuhudhuria kwa wingi katika maeneo yatakayo pitiwa na mwenge lakini pia katika eneo la mapokezi na eneo la mkesha wa mwenge, Mwisho timu ilifanya tathmini ya miradi yote na kuwataka wataalamu wa Halmashauri kuendelea kujiandaa vyema kuelekea kwenye mapokezi ya mwenge wa Uhuru.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.