Mafunzo ya siku tano yamefanyika kuanzia tarehe 20 April 2021 hadi 24 April 2021 kwa wawezeshaji ambao watahusika kwa lengo la kuibua kaya maskini kwenye vijiji vya Halmashauri ya Mtama. Mafunzo hayo yamesimamiwa na Madam Graceana Maganga kutoka TASAF kanda ya Dar es Salaam kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa TASAF Makao makuu. Katika hotuba ya ufunguzi, Mhe, Thomas Safari kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Lindi, amesisitiza suala zima la kuibua kaya zenye sifa kulingana na vigezo vilivyopo. Aidha kufanya kazi kwa uadilifu ili kutenda haki ya kuwapatia kipato wale wote wanaohusika. Huu ni utekelezaji wa malengo ya TASAF kipindi cha Pili cha awamu ya tatu. "PAMOJA TUONDOE UMASKINI".
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.